WORLD VISION
Majimbo ya Mto Wami katika eneo la bonde la mto Wami, ambalo linajumuisha eneo la wakazi wa takriban milioni 1.8, linahitaji utunzaji wa vyanzo vya maji na mazingira ili kuhakikisha upatikanaji wa maji safi na ya kutosha kwa wakazi.
2009 · 2 pages

Abstract
Juhudi za sasa za utunzaji wa vyanzo vya maji na mazingira, ikiwemo upandaji wa miti, zimeanzishwa ili kuhifadhi vyanzo vya maji na mazingira. Changamoto kubwa katika vijiji vya eneo hilo ni upatikanaji wa maji safi na salama kwa wakazi. Hii inahitaji kuhifadhi na kutunza vyanzo vya maji na mazingira ili kuwa endelevu. Pia, kufuata kanuni za usafi wa mazingira kwa ajili ya afya ya jamii ni muhimu. Ofisi ya Maji Bonde la Wami/Ruvu na Tanzania Coastal Management Partnership (TCMP) kwa kushirikiana na wadau mbalimbali katika bonde huo, walifanya kazi kwa pamoja ili kukabiliana na baadhi ya changamoto hizi kwa kutumia ufadhili uliotoka kwa muungano wa Wadau wa Maji na Maendeleo (WADA). Elimu ya Afya Mashuleni ni sehemu muhimu ya mradi huo. Shule nyingi zinazojengwa zimekuwa hazina miundombinu mizuri ya vyoo pamoja na uhaba wa maji kwa wanafunzi na walimu. Ujenzi wa vyoo mashuleni na katika maeneo ya makazi ya watu wengi ulifanyika katika vijiji vya Dumila, Msowero, Madizini, Hale na Miono, ili maeneo mengine yaweze kuiga. Kuna shule ambazo zilikaribia kufungwa kutokana na ukosefu wa vyoo. Tathmini ya mahitaji ya Maji kwa ajili ya watu na Mazingira ilifanywa na timu ya wataalam washauri wa fani mbalimbali mwezi Aprili 2007. Timu hiyo ilikusanya takwimu/taarifa mbali mbali katika mto Wami ili kuzifanyia uchambuzi wa kina kwa kusudi la kufahamu hali halisi ya afya ya mto na rasilimali zilizopo na uwezo wake wa kukidhi mahitaji mbali mbali ya watu na mazingira. Mipango ya upandaji miti na vitalu vya miche, ulipokelewa vyema na wananchi, ni mfano mzuri wa kuigwa. Hata hivyo, kazi zaidi zinahitajika kufanyika katika Bonde la Mto Wami ili kuhifadhi rasilimali za maji na mazingira. Kilimo cha umwagiliaji mkubwa na shughuli za Viwanda huzuza majitaka ambayo humwagwa kwenye mito na kuharibu ubora wa maji yake. Hali hii inahatarisha afya za wananchi pamoja na viumbe hai vya majini. Kwa hiyo, wataalamu kwa kushirikiana na Viwanda vya Mtibwa na Kigombe wanatayarisha mpango wa kupunguza matumizi ya maji pamoja na uchafuzi wa vyanzo vya maji.
Connected topics
Classification
USAID DEC