USAID
Unasihi na Unasihi Elekezi ni mbinu muhimu katika kukuza tija na ufanisi mahali pa kazi na ni za lazima katika muktadha wa elimu Tanzania.
2019 · 16 pages

Abstract
Baadhi ya viongozi na wasimamizi wa elimu katika nyakati mbalimbali wamekuwa wakifanya unasihi na unasihi elekezi kama sehemu ya kukuza ufahamu na utendaji wa walimu katika ngazi ya shule. Ni muhimu Unasihi na Unasihi Elekezi kuwa endelevu katika shule zote. Unasihi (Mentoring) ni ushawishi wa mtu kwa mtu mwingine kutokana na tabia, mwenendo na utaalamu wa mnasihi. Katika shule, Unasihi unajiri pale mwalimu au mfanyakazi mwenye ujuzi na uzoefu zaidi ya mwalimu/mfanyakazi mwingine anapomwongoza na kumshawishi kuhusu mwenendo na njia bora zaidi za kumwezesha mnasihiwa kuwa bora katika weledi na ufanisi kazini. Unasihi elekezi (Coaching) ni kufundisha/kuhaulisha stadi fulani kwa mtu mwingine kutokana na uzoefu alionao mnasihi. Unasihi elekezi unataka mnasihi elekezi na mnasihiwa kuwa katika sehemu moja kwa wakati mmoja na kawaida ni wa muda mfupi. Baadhi ya vielazo vya mfanano na tofauti kati ya Unasihi na Unasihi Elekezi vimeainishwa katika jedwali lifuatalo. Mbinu za Unasihi na Unasihi Elekezi ni tofauti. Unasihi Elekezi unalenga kuboresha ufundishaji wa mwalimu au kumshawishi mwalimu kupata mafanikio zaidi katika kufundisha. Unasihi, kwa upande mwingine, unalenga ukuzaji endelevu wa matamanio ya mwalimu kuhusu taaluma na utaalamu wa ualimu. Unasihi unaweza kufanyika ili kufanya rekebisho fulani, ilhali Unasihi Elekezi sio kwa ajili ya rekebisho tu. Muda wa Unasihi Elekezi ni mfupi au wa kati, ilhali Unasihi unaweza kufanyika kwa muda mrefu. Mkakati wa Unasihi Elekezi ni utatuzi wa pamoja wa changamoto na ubainishaji wa fursa ya kujitathmini, kujifunza na kukuza stadi mpya. Unasihi, kwa upande mwingine, unalenga kuwa rafiki, kuongeza utambuzi, kuchunguza mbadala, kushirikisha uzoefu. Stadi za kukabiliana na watu ni muhimu zaidi katika Unasihi, ilhali umahiri ni muhimu zaidi katika Unasihi Elekezi. Matokeo ya Unasihi Elekezi ni ongezeko la matokeo ya jumla ya ufundishaji, ongezeko la uwezo wa kufanya kazi kwa kujitegemea wakati wa changamoto mpya, na ongezeko la kujitambua na maarifa. Unasihi unahitaji mnasihi kuwa na stadi mbalimbali ili kufanya kazi kwa ufanisi. Baadhi ya stadi hizi ni uwezo wa kusikiliza kwa umakini na kuelewa, kuelewa mazingira ya kufundishia na mahitaji maalumu kwa makundi mbalimbali ya ujifunzaji, kujenga uaminifu, uwezo wa kuweka malengo ili kumwezesha mnasihiwa kuwa na uwezo wa kujiwekea malengo, kuwapa motisha chanya, uwezo wa kutoa mrejesho chanya na mahususi, uwezo wa kujenga mahusiano chanya, kujitambua na kujiheshimu, unyumbufu wa kusikiliza
Connected topics
Classification