RTI INTERNATIONAL
Ufahamu wa Fonimu ni mchakato wa kufahamu, kutambua, na kutumia sauti tofauti tofauti za sauti zikiwa pamoja au zikiwa kwenye silabi au neno.
10 pages

Abstract
Ufahamu huu ni muhimu kwa mwanafunzi kusoma na kutamka maneno. Ufahamu wa Fonimu unajumuisha uwezo wa kutambua sauti husika katika neno, kama vile sauti ya kwanza, sauti ya mwisho, na sauti ya kati. Ufahamu wa Fonimu unaweza kugawanywa katika sehemu nne: maneno, silabi, sauti za kipekee katika neno, na mianzo na miisho ya maneno tofauti tofauti. Sehemu hizi zote nne hufunzwa bila kuandika chochote na huhusisha sauti pekee. Ufahamu wa Fonimu ni muhimu kwa mwanafunzi kusoma na kutamka maneno. Ufahamu huu unaweza kudhihirisha kumwezesha mwanafunzi kuweza kujifunza kusoma. Ufahamu wa Fonimu na utambuzi wa fonimu hufanya kazi kwa pamoja na hutegemeana pakubwa. Ufahamu wa Fonimu unaweza kufanywa kwa kufunza sauti husika mwanzoni mwa neno, kisha mwishoni mwa neno, na kumalizia kwa kutambua sauti husika katikati mwa neno. Mwalimu pia anaweza kusoma maneno mawili na kuwauliza wanafunzi iwapo sauti zake ni sawa au tofauti. Ufahamu wa Fon
Connected topics
Classification

USAID DEC