RTI INTERNATIONAL
Kato na Amina wanaishi mjini na wazazi wao.
222 pages

Abstract
Baba yao hufanya kazi viwandani. Wakati wa likizo, mama yao aliwapeleka mashambani kuwatembelea jamaa zao. Amina na Kato walijawa na furaha tele. Walipofika mashambani, walimkuta babu yao akilisha ng'ombe na mbuzi wake. Walifurahi sana kumuona babu. Babu alimshika bata na kuwachinjia Amina na Kato. Aliwapakulia kitoweo kitamu kwenye bakuli lililokuwa kubwa sana. Jioni, baba yao mdogo alifika nyumbani kwa babu. Aliwapeleka Kato na Amina kuwachukua mbuzi wake kutoka malishoni. Wakati wa jioni, shangazi yao aliwatembelea nyumbani kwa babu. Shangazi aliwaletea paka wa kuwashika panya. Asubuhi ilipofika, shangazi aliwapa chai kwa birika. Pia, aliwapa viazi vitamu kwa sahani safi. Wakati wa mchana, Amina na Kato walitembea shambani mwa babu. Waliwaona bata, punda, nguruwe, na mbwa uwanjani. Kato na Amina wanaishi mjini na wazazi wao. Babu yao alikuwa akilisha ng'ombe na mbuzi wake shambani. Babu alimshika bata na kuwachinjia Amina na Kato. Kato na Amina walichinjiwa kitoweo kitamu kwenye bakuli lililokuwa kubwa sana. Baba yao mdogo alipeleka Kato na Amina kuwachukua mbuzi wake kutoka malishoni. Kato na Amina walipelekwa kuwachukua mbuzi wake kutoka malishoni. Kato na Amina waliona bata, punda, nguruwe, na mbwa uwanjani shambani mwa babu.
Connected topics
Classification
USAID DEC