USAID
Mwongozo wa Mwalimu wa Kiswahili kwa Darasa la 3 umekuwa na mwendelezo wa herufi na sauti kutoka kwa darasa la 2.
2018 · 177 pages

Abstract
Mbinu hii inahusisha kusoma maneno magumu zaidi yenye uwiano tata kati ya herufi na sauti. Matini kwenye masomo yanawiana kimandhari na silibasi ya Taasisi ya Mitaala ya Kenya na yameundwa kwa uangalifu ili kumfidua mwanafunzi kwa aina tofauti ya maandishi huku pia yikitilia maanani misamiati ya kimandhari. Kila matini inajumuisha mifumo ya maneno na miundo husika ya lugha. Ili kuboresha ufahamu wa wanafunzi wa matini, baadhi ya mbinu za ufahamu zinazolingana na kiwango chake zimetumiwa ili kumpa mwanafunzi mbinu tofauti za kuelewa matini. Katika darasa la 3, mwanafunzi anafunzwa kutumia hatua tano katika mchakato wa kuandika. Hatua hizi ni kabla ya kuandika/kupanga, kuandika nakala ya kwanza, kuhakiki, kurejelea na kuchapisha. Kila hatua hufunzwa kwa wiki moja. Mbinu hii hutoa nafasi kwa mwanafunzi kufanya mazoezi ya kila hatua kwenye mchakato huku wakikuza uwezo wa kuandika insha bila msaidizi. Kila mpango wa somo unajumuisha shughuli tofauti zilizopangwa ili kukuza ujuzi na ufahamu wa mwanafunzi wa lugha ya Kiswahili. Shughuli za somo ni simulizi na za kuandika zikizingatia stadi nne za lugha (kusikiliza, kuzungumza, kusoma na kuandika). Katika masomo manne ya kwanza, wanafunzi hujifunza na kufanya mazoezi ya matumizi ya maneno, kusoma hadithi, ufahamu na sarufi. Somo la tano linazingatia marejeleo na shughuli za kutathmini zitakazosaidia mwalimu kufuatiliza maendeleo ya mwanafunzi. Mbinu hii inahusisha kutumia mbinu tofauti za ufahamu ili kumpa mwanafunzi ufahamu wa matini. Mwongozo huu wa mwalimu umekuwa na maelekezo ya wataalamu wa kimataifa na wa hapa nchini wa kusoma na wa lugha kwa kufuata mchakato uliopangwa kwa utaratibu. Mbinu hii inahusisha kutumia mbinu tofauti za ufahamu ili kumpa mwanafunzi ufahamu wa matini. Mwongozo huu umekuwa na maelekezo ya wataalamu wa kimataifa na wa hapa nchini wa kusoma na wa lugha kwa kufuata mchakato uliopangwa kwa utaratibu.
Connected topics
Classification

USAID DEC