RTI INTERNATIONAL
Kusikiliza na kuzungumza ni kipengele muhimu cha lugha ambacho kinahusisha kuelewa na kutumia lugha katika muktadha wa kawaida.
16 pages

Abstract
Lugha zungumzwa ni sehemu ya lugha zote na hutumika katika kujieleza na kuwasilisha hisia, maoni na ujuzi ambao tunayo. Lugha zungumzwa hukuzwa kadri mtoto anavyokua na kutangamana na mazingira yake. Vipengele vya lugha zungumzwa ni vitano: stadi za kifonolojia, sintaksia, mofolojia, pragimatiki, na semantiki. Stadi za kifonolojia ni ufahamu wa sauti katika lugha, ambayo inajumuisha silabi na vina. Sintaksia ni sheria zinazohusu matumizi ya lugha kama mpangilio wa maneno na muundo wa sentensi. Mofolojia ni jinsi mofimu au vipashio vidogo vyenye maana katika neno huwekwa pamoja ili kuleta maana. Pragimatiki ni uelewa wa lugha kimuktadha hasa kwa kuzingatia sheria za lugha katika jamii husika. Semantiki ni kipengele ambacho hujulikana kama msamiati, kwa sababu huhusisha maana ya maneno katika lugha. Kuwa na umilisi wa lugha zungumzwa humwezesha mwanafunzi kuelewa anachosoma. Vipengele muhimu katika kufanikisha kuelewa matini ni sintaksia, pragimatiki, na msamiati/semantiki. Kulingana na utafiti, vipengele hivi vinahusiana sana na usomaji wa ufahamu. Ujuzi wa sarufi na maana ya maneno katika lugha ni muhimu sana katika kuelewa kinachosomwa. Ufahamu wa lugha inayotarajiwa kama vile lugha rasmi, legevu, na istilahi kuhusu mada maalum huboresha ufahamu na uwezo wa msomaji wa kutabiri na kutumia muktadha kama mbinu ya kuelewa matini. Kusikiliza na kuzungumza hufunzwa kwa kutumia mbinu tofauti kwa kuzingatia kila kipengele (fonolojia, sintaksia, mofolojia, pragimatiki, na semantiki) au kufunzwa kama mada moja kwa jumla. Mikakati yote ya kufunza inadhamiria kukuza lugha zungumzwa. Mikakati hii ni kama: kuwapatia wanafunzi fursa ya kujiunga na vikundi vya mijadala na maigizo darasani, kuwafikirisha wanafunzi kwa kuwauliza maswali wazi ili kuzua mijadala inayowahusisha kimaongezi, kueleza maana ya maneno hasa yanayohusu mada zinazofunzwa ili waweze kutumia maneno hayo kuwasiliana ifaavyo, na wanafunzi wanafaa kusomewa vitabu vya viwango vya juu ili waweze kukuza msamiati hata kabla ya kuanza kujisomea. Katika mbinu ya Tusome, kusikiliza na kuzungumza hufunzwa kila wakati wa kipindi kwa njia ya moja kwa moja au huhusishwa na mada nyinginezo katika gredi zote 3. Vipengele vya fonolojia, sintaksia, na mofolojia hufunzwa kwa njia isiyo ya moja kwa moja hasa wakati wanafunzi wanafanya mazoezi kimazungumzo. Zoezi la mkufunzi la ufahamu wa fonimu huboresha utambuzi wa sauti ambao ni muhimu katika usomaji wa baadaye. Msamiati ni jumla ya maneno yote katika lugha fulani. Msamiati vilevile ni maana
Connected topics
Classification