RTI INTERNATIONAL
Ufasaha ni uwezo wa kusoma matini kwa haraka, usahihi, na kuelewa ishara zinazowakilishwa na maneno.
14 pages

Abstract
Ufasaha hujengwa katika stadi za ufahamu wa kifonemiki na kanuni ya alfabeti, ambayo husaidia mwanafunzi kutambua maneno moja kwa moja na kutamka au kusoma maneno haraka. Wanafunzi wanaosoma kwa ufasaha husonga zaidi ya kusoma matini hadi kiwango cha kuelewa anachosoma na kukilinganisha na mazingira, hivyo basi kuelewa kwa haraka. Ufasaha husaidia kuelewa kinachosomwa kwa kufanya ubongo kulenga kile kinachosomwa badala ya kulenga kutamka sauti na maneno. Ufasaha husaidia kuelewa kinachosomwa kwa kwa kuufanya ubongo kulenga kile kinachosomwa badala ya kulenga kutamka sauti na maneno. Ufasaha husaidia kuelewa kinachosomwa kwa kufanya ubongo kulenga kile kinachosomwa badala ya kulenga kutamka sauti na maneno. Ufasaha huchangia pakubwa katika ujuzi wa mwanafunzi kuelewa matini. Habari tunazosoma huwekwa katika kumbukumbu za akili. Kuna aina mbili za kumbukumbu katika ubongo wa binadamu, kumbukumbu ya muda mrefu na kumbukumbu ya muda mfupi au inayofanya kazi. Kumbukumbu ya muda mrefu huifadhi habari, kuidhibiti na kuirudisha inapotakikana (retrieve) baada ya muda mrefu. Kumbukumbu ya muda mfupi ina upungufu kuwa ina kiwango cha kiasi cha habari ambazo inapaswa kuifadhi kiasi Fulani cha habari. Ufasaha husaidia kuelewa
Connected topics
Classification