WORLD HEALTH ORGANIZATION
Ugonjwa wa surua ni ugonjwa unaosababishwa na virusi aina ya "Morbillivirus paramyxovirus" vinavyoenea kwa haraka kutoka kwa mtu mmoja kwenda kwa mwingine, hasa sehemu zenye msongamano.
2014 · 3 pages

Abstract
Ugonjwa huu huathiri watu wa rika zote, lakini watoto wenye umri chini ya miaka mitano huathirika zaidi. Ugonjwa huu unaenezwa kwa njia ya hewa pale mgonjwa anapokohoa au kupiga chafya. Dalili za ugonjwa wa surua ni homa na vipele vidogo vidogo hutokea ambavyo huanza kwenye paji la uso, nyuma ya masikio na kusambaa usoni na mwili mzima. Macho pia huwa mekundu, na mafua na kikohozi huonekana. Kumbuka kwamba ikiwa mtoto anapata mojawapo ya dalili hizi, mpeleke mtoto kwenye kituo cha huduma za afya haraka kwa uchunguzi, matibabu na ushauri. Madhara ya ugonjwa wa surua ni kuhara kunaweza kusababisha upungufu wa maji na chumvi chumvi mwilini, nimonia, masikio kutoa usaha ambayo huweza kusababisha mtu kuwa kiziwi, vidonda vya macho vinavyoweza kusababisha upofu, utapiamlo, na kifo huweza kutokea. Ugonjwa wa surua kwa watoto unaweza kuzuilika kwa njia ya chanjo. Chanjo ya kwanza hutolewa sambamba na matone ya vitamini A, na mtoto anapaswa kupata chanjo hii miezi tisa. Chanjo ya pili hutolewa motto anapotimiza umri wa miezi kumi na nane (mwaka mmoja na nusu). Kampeni za chanjo pia zinatokea sambamba na chanjo ya kwanza na ya pili. Utoaji wa chanjo zote mbili za surua kwa watoto kulingana na ratiba kunawapa kinga kamili. Manufaa ya chanjo ya surua kwa mtoto ni kupunguza maradhi na madhara ya surua, kupunguza vifo vitokanavyo na surua, kupunguza gharama ya kuuguza wagonjwa wa surua, na kutokomeza ugonjwa wa surua. Ugonjwa wa surua hauna tiba, bali matibabu hutolewa kwa ajili ya kutibu madhara yaliyosababishwa na surua kama vile homa, kuhara, nimonia au masikio yenye kutoa usaha. Mtoto mwenye surua anapaswa apewe vinywaji na chakula cha kutosha. Kumbuka kwamba chanjo zote zinatolewa bila malipo katika vituo vyote vya huduma za afya.
Connected topics
Classification