RTI INTERNATIONAL
Malengo ya kufundishia katika elimu ya Kiswahili ni kutoa ujuzi na uwezo wa wanafunzi katika kusoma na kuandika.
24 pages

Abstract
Mbinu za kufundishia ni njia na mikakati ambayo mwalimu hutumia darasani ili kukuza stadi na pia mienendo ya wanafunzi. Mbinu bora ya kufundisha humsaidia mwanafunzi kupata ujuzi maarifa, stadi/uwezo, mtazamo na maadili yanayotarajiwa kwa mujibu wa malengo katika mtalaa. Kuna mbinu tofauti za ufunzaji ambazo ni mahususi katika elimu. Utafiti wa muda mrefu umedokeza mbinu kadhaa za kufundishia. Kila mbinu ina umuhimu wake na filosofia katika elimu. Mbinu hizi zinahitaji viwango tofauti vya ujuzi na nyenzo za kutosha. Mbinu hizi ni pamoja na uundaji, ufundishaji unaoelekezwa, mbinu tatuzi, ujifunzaji wa kudadisi, ufundishaji uliodhibitiwa kimaudhui, ujifunzaji wa kiushirika, ujifunzaji marika kwa zamu, na mbinu ya kufunza kwa kufanya (Ninafanya/Tunafanya/Unafanya). Mbinu ya kufunza kwa kufanya (Ninafanya/Tunafanya/Unafanya) ni mbinu inayohusisha kufundisha katika hatua fupifupi, kuwaongoza wanafunzi kufanya mazoezi ya mwanzo, na kuhakikisha kuwa kila mwanafunzi alipata mazoezi ya kutosha na ya hali ya juu. Mbinu hii inahusu kukuza stadi kutokana na kuelekezwa na mwalimu. Matumizi ya vikundi vidogo na maelezo ya ana kwa ana yanasisitizwa na mwalimu ambaye huandaa vipindi akihakikisha kwamba kila mada inafunzwa kwa mpangilio na kikamilifu. Mbinu ya kufunza kwa kufanya (Ninafanya/Tunafanya/Unafanya) inahusisha hatua sita za kufuata: 1. Aeleze umuhimu wa stadi 2. Aonyeshe wazi ni stadi gani anafunza 3. Awape mazoezi elekezi kuhusu stadi hadi wamakinike 4. Achunguze kiwango cha kufahamu na atoe marekebisho jengevu 5. Atoe mazoezi zaidi 6. Tathmini ujifunzaji mwishowe Mbinu ya kufunza kwa kufanya (Ninafanya/Tunafanya/Unafanya) ni muhimu sana hasa kwenye miktadha ambapo wanafunzi hawajapata uzoefu wa matini au hawaitumii lugha inayotumiwa darasani katika miktadha mingine. Mbinu hii inahusisha kukuza stadi kutokana na kuelekezwa na mwalimu, na inahitaji mwalimu awapatie wanafunzi fursa wafanye mazoezi ya stadi na mada waliojifunza na atoe marekebisho jengevu.
Connected topics
Classification