USAID DEC
Rotavirus ni virusi vya aina mbalimbali ambavyo huchangia kwa kiwango kikubwa katika magonjwa ya kuharisha kwa watoto walio na umri wa chini ya miaka mitano.
2012 · 29 pages

Abstract
Takwimu za mwaka 2008 zinaonyesha kuwa magonjwa ya kuharisha yasababishwayo na rotavirus yalichangia asilimia 30 – 50 kwa watoto wote wenye umri chini ya miaka mitano waliolazwa kwa ugonjwa wa kuharisha. Kiasi cha asilimia 40 ya watoto huambukizwa wakiwa na umri wa chini ya mwaka mmoja, lakini mara nyingi watoto wenye umri kati ya miezi 6 na 11 huathiriwa zaidi na ugonjwa huo. Virusi vya Rota huenezwa kwa njia ya kula au/na kunywa maji yaliyochafuliwa na kinyesi chenye virusi hivyo. Muda wa uambukizo hadi dalili za ugonjwa kujitokeza huchukua kati ya saa 24 hadi 48. Mtoto anaweza kuambukizwa zaidi ya mara tatu kabla hajatimiza miaka 3, hata hivyo uambukizo wa kwanza ni hatari zaidi. Dalili za ugonjwa ni kutapika, kuharisha, kupungukiwa maji na chumvi chumvi mwilini, na mara nyingine huambatana na homa. Kuharisha kunaweza kudumu kwa muda wa siku 4 hadi 7. Upungufu mkubwa wa maji na chumvichumvi mwilini ni madhara makubwa yatokanayo na kuharisha na yanaweza kusababisha kifo. Madhara mengine yanayoweza kutokea ni utapiamlo, kudumaa, na mtindio wa ubongo. Kunyonyesha maziwa ya mama, kuimarisha usafi wa mazingira, na kunawa mikono kwa sabuni husaidia kupunguza mambukizo ya magonjwa ya kuhara. Hata hivyo, tafiti zinaonyesha kuwa magonjwa ya kuhara yasababishwayo na Rotavirus huzuilika vizuri zaidi kwa chanjo. Tanzania imeamua kutumia chanjo ya Rotarix kukinga ugonjwa wa kuharisha unaosababishwa na vimelea vya rotavirus. Chanjo hii ubora wake umethibitishwa na Shirika la Afya Duniani (WHO). Chanjo hii inapatikana katika hali ya majimaji ndani ya kichupa kilichotengenezwa kwa ujazo wa mls 1.5, na mtoto hupewa kupitia mdomoni. Chanjo ya rotavirus ni salama haina madhara makubwa, na inaweza kutolewa pamoja na chanjo nyingine kulingana na ratiba ya chanjo za watoto bila matatizo yoyote. Mtoto aliyeipata chanjo hii anaweza kupata maudhi madogomadogo kama homa, kuharisha, kutapika, kukosa hamu ya kula, kuumwa tumbo, na wakati mwingine kujamba mara kwa mara. Chanjo hii inahifadhiwa katika nyuzi joto +2⁰C hadi +8⁰C, kama chanjoya Pentavalent. Hairuhusiwi kugandishwa, kama ikiganda itapoteza ubora wake na hairuhusiwi kutumika. Tunza chanjo katika jokofu kwenye nyuzi joto +2°C hadi +8°C. Usiache chanjo hii kuganda. Hatua za kufungua chanjo ni kama ifuatavyo: Ondoa kifuniko cha chupa ya chanjo, kisha gonga gonga kwa kutumia kidole kuteremsha chanjo sehemu ya juu ya kichupa. Geuza kifuniko cha kichupa juu chini, halafu weka mahali p
Connected topics
Classification
2016USAID DEC