USAID DEC
Kanuni ya Alfabeti ni muhimu katika usomaji na kusoma maneno.
15 pages

Abstract
Ina maana kwamba herufi huwakilisha sauti ambazo huunda maneno. Kanuni hii ni muhimu kwa mwanafunzi kwa sababu inasaidia kuendeleza maneno vizuri na kujieleza kimaandishi. Mwanafunzi anahitaji kuwa na ufahamu wa sauti wa kila herufi na uwezo wa kuziweka sauti hizi pamoja ili kusoma silabi, kisha na neno. Wanafunzi wanapaswa kujua jina la herufi na sauti ya kila herufi, jinsi ya kutenganisha maneno yaliyoandikwa katika herufi, na sauti ili kuweza kusoma maneno. Stadi hii ya kutumia sauti kuunda maneno katika lugha ya Kiingereza na kutumia silabi kuunda maneno katika lugha ya Kiswahili inaitwa kusimbua. Lugha ya Kiingereza ni gumu na kwa hivyo wanafunzi wanapaswa kufunzwa kuanzia sauti zile rahisi hadi zile gumu. Kanuni ya Alfabeti pia inahusisha kutambua herufi changamano, ambazo ni muungano wa sauti mbili au zaidi katika huku kila herufi ikiifadhi sauti yake katika neno hilo. Mara nyingi herufi hizi hutokea mwanzoni au mwisho wa neno katika lugha ya Kiingereza. Katika lugha ya Kiswahili, herufi changamano hutokea mwanzoni mwa maneno. Pia, kanuni ya Alfabeti inahusisha kutambua herufi mwambatano, ambazo ni kikundi cha herufi mbili zinazofuatana na ambazo zinawakilisha sauti moja. Wanafunzi hawapaswi kutamka sauti moja, bali sauti mbili. Kufunza kanuni ya Alfabeti kunapaswa kuanzia herufi kubwa na ndogo, na kuhakikisha kuwa umefunza waziwazi jina na sauti ya herufi na kuonyesha uhusiano wake. Ni vyema pia kutambua sauti ambazo zinafanana kisauti katika lugha ya Kiswahili na pia Kiingereza. Kanuni ya Alfabeti ni muhimu kwa mwanafunzi kwa sababu inasaidia kuendeleza maneno vizuri na kujieleza kimaandishi. Mwanafunzi anahitaji kuwa na ufahamu wa sauti wa kila herufi na uwezo wa kuziweka sauti hizi pamoja ili kusoma silabi, kisha na neno.
Connected topics
Classification